NA HERI SHAABAN (CCM ILALA)
DIWANI KATA ya Ilala Saady Kimji, amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM ya kipindi cha January mpaka Juni 2026.
DIWANI Saady Khimji, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama amesema kwa kipindi cha miezi sita kata ya Ilala anafanya mambo makubwa ina kuwa kata ya kisasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ,kwa kushirikiana pamoja na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani Kimji alitaja baadhi ya mambo aliyotekeleza kipindi cha miezi sita ikiwemo afya na mazingira, ujenzi wa Zahanati ya Bunguni,mapokezi ya vifaa mbalimbali ya vifaa vya Zahanati ya Kisasa Bungoni, uzoaji wa Takataka ngumu,maji taka na maji safi,lishe, ulinzi na usalama, sekta ya Elimu msingi na Elimu Sekondari,maendeleo ya jamii na miundombinu ya Barabara.
Akizungumzia sekta ya afya amesema Zahanati ya Ilala Bungoni, ujenzi wa vyoo vya nje unaendelea ambapo kunajengwa matundu matatu ya vyoo na choo cha watu wa makundi maalum, ujenzi wa stoo,mnara wa tanki, na ujenzi wa fensi.
"Nawashukuru Wajumbe wote wa kata ya Ilala walipiga kira kwa wingi pamoka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu wa Rais wabunge na madiwani ambapo ushindi mkubwa ccm umepatikana Ilala kura za Rais Dkt.Samia pamoja na Mbunge wetu Musa Zungu ambapo CCM imeibuka kidedea "amesema Kimji.
Diwani Saady Kimji, akizungumzia katika sekta ya Elimu amesema Ilala ina shule ya msingi saba na shule za Sekondari tano,kati ya hizo shule tatu za sekondari za Serikali na shule nne za msingi za Serikali na tatu za binasfi
Diwani Kimji amesema shule ya Msimbazi Mseto imefanikiwa kupata mradi wa madarasa matatu mradi umekamilika na Sehemu zingine wako katika hatua za mwisho gharama za mradi bilioni 217,000,000/=shule ya msingi Ilala shilingi milioni 30,000,000,ukarabati madarasa mawili pamoja na shule ya msingi Mkoani vyumba sita naOfisi ya mwalimu mkuu gharama za mradi shilingi 90,000 ,0000/=
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Ilala, Habib Nasser ametumia fursa hiyo kumpongeza Diwani wa Kata ya Ilala Saady Kimji kwa kuwasilisha Ilani ya chama pamoja na kumpongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza Miradi mikubwa ya maendeleo Ilala.
Mwenyekiti Habibu Nasser katika hatua nyingine aliwataka Aliwataka Watendaji wa kata ya Ilala, pamoja na watumishi wake aliwataka wafanye kazi kwa weledi kwa kushirikiana na chama na Serikali sambamba na kutatua kero za wananchi.






Post a Comment