DKT MUNISH : MAHUSIANO MAZURI ULETWA NA MAZINGIRA WEZESHI KWA JAMII

............

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Dkt. Eveline Munisi, amesema mahusiano mazuri kati ya wananchi, taasisi na wadau mbalimbali ni msingi muhimu wa maendeleo ya taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba, Julai 5, 2026. Dkt. Munisi alisema Ofisi ya Waziri Mkuu inaendelea kushirikiana na taasisi za kijamii, taasisi za kidini, vyama vya siasa na asasi za kiraia ili kujenga umoja na mshikamano nchini.

Alisema jamii yenye mahusiano mazuri hujenga mazingira wezeshi ya maendeleo, hivyo akatoa wito kwa Watanzania kuendelea kudumisha ushirikiano, umoja na mshikamano kwa manufaa ya taifa.

Aidha, alisema Serikali inaendelea kuwekeza katika maendeleo ya ujuzi kwa vijana kupitia programu mbalimbali za mafunzo, akibainisha kuwa lengo ni kuhakikisha Tanzania inazalisha wataalamu wake na kuondoa utegemezi wa wataalamu kutoka nje ya nchi kwa miaka ijayo.

Dkt. Munisi pia aliwahimiza wananchi kutembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) katika Maonesho ya Sabasaba ili kupata elimu na huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo.

 

0/Post a Comment/Comments