HOSPITAL YA OCEAN ROAD IMEJIPANGA KUDHIBITI UGONJWA WA SARATANI

......

Na Ester Maile Dar es salam

Mkurugenzi m

Mkurugenzi Mtendaji wa hospital ya Ocean road amesema hali ya ugonjwa wa saratani bado siyo nzuri kutokana na ongezeko la wagonjwa milioni ishirini duniani na milioni kumi wamepoteza maisha.

 Amesema kwa Tanzania takwimu bado sio nzuri ambapo kumekuwa na wagonjwa elfu hamsini na vifo elfu therathini kwa kipindi cha mwaka juzi.

Dkt Msemo ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam . 

Aidha amesema kuwa kwa kipindi hiki cha sabasaba hospital ya Ocean road imepima wananchi 500 ambapo wanawake 300 wameweza kupima saratani ya Shingo ya kizazi na matiti na wanaume 200 wamepima saratani ya tezi dume hali ambayo inaonyesha kuwa wananchi kuwa na mwitikio wa kipima uhonjwa wa saratani .

Vil vile hospital ya Ocean road imejipanga kuwa na mkakati wa kudhibiti ugonjwa saratani kwa miaka kumi ambapo imejipanga kuanzisha kituo kikubwa ambacho kitasaidia wananchi kupata huduma.



 

0/Post a Comment/Comments