KAFULILA MTAALAM HITAJIKA PPP - MZUMBE (MBEYA)


******

Mhadhara wa umma unaofanyika katika Chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Mbeya umehudhuriwa na wataalamu na wanazuoni mbalimbali ambapo Mhadhiri wa chuo hiko kutoka Idara ya Mafunzo ya Biashara na Mtaalam wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), Dkt. Jasinta Msamula amemuelezea Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP-Centre), David Kafulila, kama mtaalamu mwenye uzoefu mkubwa katika masuala ya usimamizi na utekelezaji wa miradi ya ubia.

Akizungumza katika utambulisho huo, Dkt. Jasinta amebainisha kuwa Kafulila ana uelewa mpana kuhusu mifumo ya PPP na mchango wake katika kuunganisha nguvu kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ili kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.

Mhadhara huo umebeba mada kuu isemayo “Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) kama chachu ya kufikia malengo ya Dira 2050”, ambapo washiriki wamepata fursa ya kujadili nafasi ya PPP katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo na uboreshaji wa huduma za kijamii.

Kafulila ameelezwa kuwa miongoni mwa wataalamu wanaoendelea kuhamasisha matumizi ya PPP kama nyenzo ya kupunguza mzigo wa uwekezaji kwa serikali, huku ikiimarisha ushiriki wa sekta binafsi katika kukuza uchumi na kufanikisha malengo ya muda mrefu ya taifa.






Mwisho.

0/Post a Comment/Comments