Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas Tanzania Benoite Araman(kulia) Meneja miradi nishati safi ya kupikia Jennifer Mosha, Skauti Mkuu Tanzania Rashid Mchata(wa pili kushoto) pamoja na Kamishina Mkuu wa Skauti Tanzania Abubakari Mtitu wakikata utepe kuzinduzi Kitabu cha Mwongozo wa matumizi salama nishati safi ya kupikia ya LPG. Uzinduzi huo umefanyika leo Julai 15,2025 jijini Dar es Salaam.
.........
Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Limited kwa Kushirikiana na Chama cha Skauti Tanzania leo Julai 15, 2026 wameanza Safari ya Ushirikiano unaolenga kutoa Elimu ya usalama wa gesi ya LPG, kuimarisha maandalizi ya kukabiliana na dharura, na kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia stadi na fursa za ajira.
Hafla ya utiaji saini imefanyika Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi waandamizi wa taasisi zote mbili, wakiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas Tanzania, Benoite Aramani, na Kamishna Mkuu wa Chama cha Skauti, Rashid Mchata.
Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas Tanzania Benoite Aramani amesema ushirikiano huo unaenda zaidi ya kusambaza gesi.
"Katika Oryx tunaamini upatikanaji wa nishati safi unapaswa kuambatana na elimu, usalama na fursa kwa vijana, Kwa kushirikiana na Skauti ambao wana mtandao mkubwa kitaifa, tunaweza kufikia jamii nyingi na kuleta mabadiliko ya kweli" amesema Aramani.
Kwa upande wake, Kamishna Mkuu Mchata alieleza kuwa ushirikiano huo ni daraja la fursa kwa vijana.
"Tanzania Scouts Association haikubali kuwa mtazamaji wa maendeleo, Sisi ni sehemu ya suluhisho, Kupitia makubaliano haya tutatoa elimu kwa maelfu ya wananchi na kuwajengea vijana uwezo wa kutambua na kuzalisha fursa" ameeleza Mchata.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na pande zote mbili, ushirikiano huu utatekelezwa kwa kutoa elimu ya usalama wa LPG katika shule zaidi ya 200 na kwa wanajamii 10,000 kupitia kampeni na mafunzo ya vitendo ndani ya mwaka mmoja.
Pia mpango utajumuisha kuwafundisha Skauti 500 ujuzi wa kukabiliana na dharura pamoja na kufanya mazoezi 12 ya jamii kila mwaka, huku kukiwa na programu maalum kwa vijana 300 katika utunzaji wa LPG, ukaguzi wa mitungi na matengenezo ambapo watapata vyeti na kuunganishwa na fursa za uanagenzi na ajira.











Post a Comment