Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametuma salamu za pole kwa Amir wa Qatar, Serikali na wananchi wa Qatar kufuatia kifo cha Amir wa zamani wa Taifa hilo, Hayati Sheikh Hamad bin Khalifa Al Thani.
Rais Dkt. Mwinyi ametoa salamu hizo za pole leo, tarehe 21 Julai 2026, alipofika katika Ubalozi wa Qatar nchini Tanzania, uliopo Oysterbay, jijini Dar es Salaam, na kusaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha kiongozi huyo.
Akiwa ubalozini hapo, Rais Dkt. Mwinyi, kupitia kwa Balozi wa Qatar nchini Tanzania, Mhe. Fahad Rashid Al-Muraikhi, ametoa salamu za pole kwa Amir wa Qatar, Mhe. Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, familia ya kifalme, Serikali na wananchi wa Qatar kutokana na msiba huo mkubwa.
Amesema Hayati Sheikh Hamad ataendelea kukumbukwa kwa uongozi wake wenye maono, mchango wake katika maendeleo ya Qatar na juhudi zake za kuimarisha elimu, uchumi, ustawi wa wananchi na nafasi ya Taifa hilo katika masuala ya kimataifa.
Hayati Sheikh Hamad bin Khalifa Al Thani alifariki dunia tarehe 12 Julai 2026, akiwa na umri wa miaka 74.






Post a Comment