RAIS MWINYI ASHUHUDIA REA IKITWAA TUZO YA MUONESHAJI BORA WA TAASISI ZA SERIKALI



📍 Dar es Salaam

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameshuhudia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ukitwaa Tuzo ya Muoneshaji Bora wa Taasisi za Serikali (*Government Institutions Exhibitor*) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) 2026.

Tuzo hiyo imepokelewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma wa REA, Bi. Martha Chassama, kwa niaba ya Wakala.

REA inawashukuru wadau wote waliotembelea banda lake, kujionea mafanikio na utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini, pamoja na kuendelea kuunga mkono jitihada za Wakala za kupeleka nishati ya umeme kwenye vitongoji. 


Mwisho
 

0/Post a Comment/Comments