RAIS SAMIA AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA MASHUJAA

.....

Na Ester Maile Dodoma 

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 25 Julai, 2026 ameongoza sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa zilizofanyika kitaifa jijini Dodoma huku Mizinga ikipigwa kuenzi maisha ya mashujaa hao

Maadhimisho hayo yamefanyika katika Uwanja wa Mashujaa uliopo Mji wa Serikali, Mtumba, ikiwa ni utamaduni wa kila mwaka wa kuwaenzi mashujaa waliopoteza maisha wakitetea na kulinda uhuru na amani ya nchi ikiwemo waliopoteza maisha katika vita vya Kagera

Katika maadhimisho hayo, Rais Dkt Samia suluhu, ameweka shada la maua kwenye Mnara wa Mashujaa, Ngao na Mkuki kama ishara ya heshima kwa waliopigania taifa lakini pia ikiwa ni desturi za kijeshi za kuwaenzi wapiganaji wetu

Viongozi Waliohudhuria Kumbukumbu hiyo nipamoja na Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi, Makamu wa Rais Emmanuel Nchimbi, Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba,

Wengine ni pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania General Jakob Mkunda, Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe Nyansaho pamoja na viongozi waandamizi wa serikali na vyombo vya ulinzi na usalama

Hapo Jana, Mwenge wa Mashujaa uliwashwa katika kuenzi mashujaa ha Wanajeshi walioshiriki Vita vya Kagera vilivyoipatia Tanzania Ushindi dhidi ya Adui Nduli Idd Amin Dada wa uganda wakaeleza namna walivyo shiriki kwenye vitahiyo

 

0/Post a Comment/Comments