********
Shirikisho la Hija Tanzania (TAHAFE) limewataka mahujaji watarajiwa na taasisi zinazoratibu safari za Hija kuhakikisha wanalipia huduma zote muhimu kwa wakati ili kuepuka changamoto za maandalizi ya safari nchini Saudi Arabia.
Naibu Katibu wa TAHAFE, Sheikh Muhammad Ali Mshangama, amesema mfumo mpya wa usajili unatoa kipaumbele kwa ulipaji wa mapema wa gharama za malazi, mahema, location na huduma nyingine zinazohitajika wakati wa ibada ya Hija.
Amesema taasisi na mahujaji wanapaswa kukamilisha malipo hayo kabla ya Agosti 13, 2027, kufuatia ratiba iliyowekwa na Wizara ya Hija ya Saudi Arabia kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa Hija.
Kwa upande mwingine, BITHA-BARA na TAHAFE zimewasisitiza Watanzania wanaokusudia kwenda Hija mwaka 2027 kutumia taasisi na mawakala walioidhinishwa pekee ili kujikinga dhidi ya matapeli.
TAHAFE pia imetangaza kuwa taasisi 16 zimeidhinishwa rasmi kusafirisha mahujaji wa Tanzania Bara, huku taasisi tatu zikiendelea na mchakato wa kupata idhini.
Wakati huo huo, Kongamano na Maonesho ya Hajj 2027 yatafanyika Agosti 15 katika Ukumbi wa Lamada, Ilala, Dar es Salaam, yakitoa elimu kuhusu Hija na huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi za Hija kutoka Tanzania na Saudi Arabia.




Post a Comment