Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho amesema umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania ni msingi muhimu wa kujenga Taifa imara na kufanikisha maendeleo ya nchi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF Cup 2026) yaliyofanyika Julai 13, 2026 katika Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam, Dkt. Nyansaho amesema mshikamano ndio nguzo itakayowezesha Taifa kusonga mbele kwa amani na maendeleo.
Amesema mashindano hayo yenye kaulimbiu ya “Umoja, Amani na Mshikamano kwa Ujenzi wa Taifa Letu Imara” yana nafasi ya kuimarisha ushirikiano ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama, huku yakikumbusha umuhimu wa kuwa kitu kimoja katika kulinda amani ya nchi.
Dkt. Nyansaho amesisitiza kuwa ulinzi wa Taifa si jukumu la Jeshi pekee wala vyombo vya ulinzi na usalama, bali ni wajibu wa kila mwananchi kushiriki katika kudumisha amani, umoja na mshikamano wa Taifa.
Kuhusu umoja na mshikamano wa kitaifa, Waziri huyo wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa amesema
"Tukiwa na umoja na mshikamano ndio kitu pekee kitakachotufanya sisi kama nchi tujenge Taifa letu imara na kuleta maendeleo. Michezo hii inatukumbusha kuwa pamoja na kutokea katika kamandi tofauti, sisi ni kitu kimoja chenye jukumu la kulinda amani na usalama wa nchi yetu.”








Post a Comment