WANACHAMA WA JOWUTA WAJIUNGA HIFADHI SCHEME YA NSSF

..........

Na Heri Shaaban(Dar es Salaam)

WANACHAMA wa Chama cha Wafanyakazi wa vyombo vya habari Tanzania (JOWUTA) wamejiunga hifadhi SCHEME ya NSSF Mkoa Dar es Salaam. 

Waandishi wa habari hao wa JOWUTA kutoka mkoa Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani walijiunga na hifadhi Scheme hiyo ya hifadhi ya jamii NSSF mwishoni mwa wiki katika mafunzo maalum ya elimu ya hifadhi ya jamii kwa waandishi wa habari iliyoandaliwa na chama cha wafanyakazi wa vyombo vya habari JOWUTA kwa kushirikiana na NSSF ili waweze kuweka akiba yao wanufaike na mafao ya NSSF. 

Akizungumza Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa vyombo vya habari Tanzania JOWUTA Selemani Msuya,amesema JOWUTA ina wanachama zaidi ya 500 Tanzania nzima fursa hiyo ya mafunzo imeanza mkoa Dar es Salaam na Pwani kwa Waandishi wa habari .

Katibu Msuya, amesema asilimia 80 ya waandishi wa habari hawana NSSF wala mfuko wa hifadhi ya jamii ambapo amesema mafunzo hayo ni muhimu na ameshauri yawe endelevu kwa waandishi wa habari wa JOWUTA wa mikoni.

Msuya aliwataka wanachama wa JOWUTA kwenda kuwa mabalozi kutoa elimu hiyo waliopata kwa jamii umuhimu wa hifadhi Scheme ya NSSF. 

Kwa upande wake mgeni rasmi mwakirishi wa Katibu Mkuu wa TUCTA, ambaye ni Mweka Hazina wa chama cha Wafanyakazi TUCTA Tanzania CPA Dkt. James Karanje amesema waandishi wa habari na Waajiri wao nchini wametakiwa kuchukua hatua ya kujiunga na mfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii NSSF ili kujenga uhakika ya maisha yao ya baadae ya kujikinga dhidi ya changamoto za kiuchumi wanapostafu au wanapopoteza uwezo wao wa kufanya kazi.

Dkt. Karanje amesema,takwimu zisizo rasmi, zinaonyesha kuwa asilimia 70 ya Wafanyakazi wa sekta ya habari hawajajiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii ambapo amesema mpango wa NSSF unatoa fursa kwa wafanyakazi wa sekta binafsi na waliojiajiri kuweka akiba kulingana na uwezo wao.

"NSSF ina manufaa mbalimbali kwa ajili ya mafao ikiwemo pesheni na huduma za bima ya afya,hivyo kuimalisha ustawi wa familia "amesema Karanje. 

Meneja wa Mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF wilaya Kinondoni,Gerald Mkonyi ,amesema mfuko huo umejipanga kuhakikisha wana habari wanapata elimu ya kutosha kuhusiana na hifadhi ya jamii ili waweze kufanya maamuzi yatakayowaletea usalama wa maisha unapofikia umri wa kustaafu 



Mwisho


 

0/Post a Comment/Comments