WAZAZI DAR WASHAURIWA KUPELEKA VIJANA WAO FUTURE WORLD KUPATA UJUZI

******

Na Mwandishi Wetu

WAZAZI na walezi katika Jiji la Dar es Salaam wameshauriwa kupeleka watoto wao katika chuo cha Future World kilichopo Chanika na Longoni 'A' Gongolamboto, kupata ujuzi kupitia kozi mbalimbali.

Chuo hicho chenye usajili wa NACTIVET Reg:0466 CAD 282/885/01 "D"/62 kimesema kupitia Chuo hicho vijana wapata fursa ya kujiajiri au kuajiriwa.

Akizungumza leo Julai  9,2026 katika uwanja wa ODP uliopo Shule ya Sekondari Chanika wilayani Ilala jijini Dar es Salaam Ofisa Masoko wa chuo hicho David Msumba amesema lengo la chuo hicho ni kuwawezesha vijana kuwa na ujuzi.

“Future World ni chuo chenye uzoefu wa karibu miaka 30 sasa, tangu kilipoanzishwa kwenye utoaji wa Mafunzo ya ufundi stadi katika fani mbalimbali. 

“Hivi Karibuni, chuo hiki kimefungua tawi lake jipya eneo la Chanika kwa Ndevu),eneo ambalo lina mandhari bora kabisa kwa utoaji wa elimu ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa hosteli nzuri za wanafunzi.

“Vijana hasa wahitimu wa kidato cha nne mnakaribishwa chuoni au kuingia kwenye

Tovuti ya chuo na kupata fomu ya kujiunga na mafunzo uyapendayo,”amesema Msumba 

Kwa upande wa kozi zinazotolewa na chuo hicho ni ufundi wa magari na pikipiki, umeme wa majumbani,ulezi wa watoto wadogo,mafunzo ya urembo na ususi,hotel management pamoja na computer Application.



 

0/Post a Comment/Comments