Makumbusho ya Taifa la
Tanzania imeendelea kupongezwa kwa kuwa eneo muhimu la kivutio lililosheheni
historia ya Taifa na Tamaduni mbalimbali za Afrika ambazo ziliasisiwa na Hayati
Baba wa Taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere.
Akizungumza wakati alipofanya ziara ya kutembelea
Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Posta Jijini Dar es salaam Raisi na Mwasisi
wa Taasisi ya Maendeleo ya Diaspora Afrika (ADDI) Balozi Arikana
Chihombori-Quao kutoka Zimbabwe amesema katika safari yake amejionea urithi
mkubwa uliopo Tanzania.
Aidha ameipongeza Makumbusho ya Taifa kwa
kuendelea kuhifadhi historia ya Tanzania na Afrika kwani yaliyohifadhiwa
yamekuwa na mchango mkubwa katika ukombozi wa bara la afrika
Ziara hiyo
inaendelea kuimarisha nafasi ya Makumbusho ya Taifa kama kitovu cha historia,
utamaduni na urithi wa Tanzania, pamoja na kuwa daraja muhimu la kuunganisha
Tanzania na Waafrika wanaoishi nje ya bara kupitia historia na urithi wao wa
pamoja
Kwa upande wake Mhifadhi Kiongozi wa Makumbusho na
Nyuma ya Utamaduni Dr Aloyce Mwambwiga amesema kuwa ujio wa mgeni huyo ni
muendelezo wa Makumbusho kuwa eneo la Kihistoria kutokana na amejionea mchango
wa Tanzania ilivyokuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru.
Amesema kuwa ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za
kuendeleza diplomasia ya kutangaza utamaduni na urithi wa Tanzania, huku
Makumbusho ya Taifa likiwa na nafasi muhimu katika kuhifadhi, kutunza na
kuwasilisha historia na utamaduni wa taifa kwa wageni wa ndani na nje ya nchi.
Dkt Aloyce ametumia fursa hiyo kuwasisitiza watanzani kujiwekea mazoea ya kutembelea katika Makumbusho ya Taifa mara kwa mara ili waweze kujifunza uruthi wa nchi yao.
Ziara za aina hiyo inatarajiwa kuongeza uelewa na
kuvutia zaidi wageni wenye asili ya Kiafrika kutoka mataifa mbalimbali
kutembelea Makumbusho ya Taifa, ili kujifunza kuhusu chimbuko, historia,
tamaduni na urithi wa Afrika kupitia Tanzania.


.jpeg)






Post a Comment