Balozi wa Tanzania nchini Italia na Mwakilishi Mkazi katika Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Mhe. Mbarouk Nassoro Mbarouk, tarehe 4 Agosti 2026, ametembelea banda la Makumbusho ya Taifa la Tanzania katika Maonesho ya NaneNane yanayoendelea jijini Dodoma.
Akiwa katika banda hilo, Mhe. Mbarouk amepata fursa ya kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na Makumbusho ya Taifa la Tanzania pamoja na maonesho ya urithi wa historia, utamaduni na malikale yanayotangaza utalii wa urithi wa Tanzania kwa wananchi na wageni.
Mhe. Mbarouk amesema kuwa Italia ni miongoni mwa masoko yenye fursa kubwa ya kuiletea Tanzania watalii wengi, akisisitiza kuwa kuendelea kutangaza vivutio vya urithi wa historia na utamaduni kutachangia kuongeza idadi ya wageni wanaotembelea nchini.




Post a Comment