BARAZA LA MADIWANI UBUNGO LASISITIZA UKUSANYAJI WA MAPATO, UBUNIFU WA VYANZO VIPYA

........

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo limesisitiza umuhimu wa kuimarisha ukusanyaji wa mapato, kubuni vyanzo vipya vya mapato pamoja na kuhakikisha mifumo ya ukusanyaji mapato inaendelea kuwa endelevu ili kuongeza uwezo wa Halmashauri katika kutoa huduma na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi.

Msisitizo huo umetolewa leo, Agosti 11, 2026, wakati wa kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, ambacho ni kikao cha robo ya nne kwa mwaka wa fedha 2025/2026, kinachojadili ajenda mbalimbali za maendeleo na ustawi wa wananchi wa Manispaa hiyo.

Kikao hicho kimeongozwa na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Mhe. Lawrence Mlaki, na kuhudhuriwa na viongozi wa Chama Wilaya, Timu ya Menejimenti ya Halmashauri pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Mhe. Aidan Kitare, ambaye amekuwa mgeni katika kikao hicho.

Wakichangia kwa nyakati tofauti, madiwani wamesisitiza umuhimu wa Halmashauri kuendelea kubuni na kuendeleza vyanzo vipya vya mapato, sambamba na kuboresha usimamizi wa vyanzo vilivyopo ili kuongeza mapato ya ndani na kupunguza mianya ya upotevu wa mapato.

Aidha, Baraza limesisitiza umuhimu wa kuendelezwa na kuimarishwa kwa Kliniki ya Mapato iliyoanzishwa na Halmashauri, ili iwe mfumo endelevu wa kutambua changamoto za ukusanyaji mapato, kuzitatua kwa wakati na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.

Madiwani pia wameeleza umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wananchi kuhusu ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali, wakisisitiza kuwa elimu hiyo itasaidia kujenga uelewa wa wajibu wa mlipa kodi na kuongeza ulipaji wa kodi kwa hiari.

Katika kuhakikisha mapato yanakusanywa kwa ufanisi zaidi, Baraza limehimiza wataalam wa Halmashauri kuendelea kufanya ufuatiliaji wa vyanzo vya mapato katika maeneo ya biashara (site), kubaini fursa zilizopo na kuhakikisha mapato yote yanayostahili kukusanywa yanaingia katika mfumo rasmi wa Halmashauri.

Aidha, Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo Mhe. Mlaki amesisitiza juu ya magari yote kuingia katika stendi kuu ya mabasi(Magufuli)
             

0/Post a Comment/Comments