DUA MAALUM YAFANYIKA LUSHOTO TANGA KUWAKUMBUKA WALIOTANGULIA

Mkuu wa Chuo cha ufundishaji wa elimu ya Dini ya Kiislamu cha Markazi Hale Mkoani Tanga Shekh Yassin Mahmun wakati akizungumza kwenye duamaalum ya kuwaombea  mashekh,ndugu na jamaa waliotangulia mbele za haki sambamba na maulid ambayo imefanyika eneo la Jitengeni Kata ya Rangwi,Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga

 Shekh wa Kata ya Rangwi Said Ally Igande akizungumza kwenye dua maalum ya kuwaombea  mashekh,ndugu na jamaa waliotangulia mbele za haki sambamba na maulid ambayo imefanyika  tarehe 30/8/2026 katika eneo la Jitengeni Kata ya Rangwi,Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga
 Mwanafamili ya Kiduma ambao ni waratibu  wa Dua hiyo Shekh Nurdin Lyimo akizungumza kwenye dua maalum ya kuwaombea  mashekh,ndugu na jamaa waliotangulia mbele za haki sambamba na maulid ambayo imefanyika  tarehe 30/8/2026 katika eneo la Jitengeni Kata ya Rangwi,Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga

..........................

NA MUSSA KHALID

Wazazi na walezi wametakiwa kuwalea watoto wao katika malezi bora ikiwemo kuwafundisha kuwakumbukuka viongozi na ndugu zao waliotangulia ili kutengeneza kizazi kilicho bora.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Chuo cha ufundishaji wa elimu ya Dini ya Kiislamu cha Markazi Hale Mkoani Tanga Shekh Yassin Mahmun wakati akizungumza kwenye hafla ya dua maalum ya kuwaombea  mashekh,ndugu na jamaa waliotangulia mbele za haki sambamba na maulid ambayo imefanyika tarehe 30/8/2026 katika eneo la Jitengeni Kata ya Rangwi,Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga

Shekh Yassin amewasisitiza vijana kutambua kuwa mtoto mwema ni yule ambaye fikra zake zinafikiria kuwaombea wazazi wake.

Kwa upande wake Shekh wa Kata ya Rangwi Said Ally Igande amewapongeza waratibu wa dua hizo na kusisitiz akuwa na muendelezo ili jamii iweze kuelimika zaidi katika kusaidiana.

Akizungumza kwa niaba ya waratibu wa hafla hiyo Mwanafamili ya Kiduma Shekh Nurdin Lyimo ameisitiza jamii kujiwekea mazoea ya kupenda kutoa kwa ajili ya Mungu ili kuweza kuwasaidia watu wenye uhitaji.

Katika Hafla hiyo mamia ya wakati wa Mkoa wa Tanga Lushoto,Korogwe,Dar es salaam na Arusha wakiongozwa na waratibu wa ukoo wa Kiduma pia wamefanya dua ya kuliombea Taifa la Tanzania ili kudumisha amani. 

0/Post a Comment/Comments