MABONDIA 79 KUTOKA VILABU 15 KUSHIRIKI KLABU BINGWA TAIFA 2026 TANGA

********

Tanga, 25 Agosti 2026— Mashindano ya Klabu Bingwa Taifa 2026 yanaanza leo katika viwanja vya Mkwakwani, Tanga, kuanzia saa 10:00 jioni, yakihusisha jumla ya mabondia 79 kutoka katika vilabu 15 watakaowania heshima ya kuwa mabingwa wa taifa.

Mashindano hayo yanatarajiwa kutoa ushindani mkubwa na kuwa fursa muhimu kwa mabondia kuonyesha uwezo wao, huku yakilenga kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya mchezo wa ngumi nchini.

 Vilabu vitakavyoshiriki

1. Ngome

2. MMJKT

3. Magereza

4. Tanga

5. Band Coy

6. Jenelo Chande

7. Mgulani JKT

8. Mashujaa

9. Makolola

10. Jeba

11. Black Eagle

12. Mkinga

13. Handeni

14. Magereza Chuo

15. Milongo MZA


Jumla ya vilabu: 15

Jumla ya mabondia: 79

Mashindano ya kuwaandaa mabondia wa Timu ya Taifa

Mbali na kuwania ubingwa wa taifa, mashindano haya yatatumika pia kama sehemu muhimu ya kutathmini na kubaini mabondia wenye uwezo na kiwango cha juu ambao wanaweza kuwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa.

_*Washindi pamoja na mabondia watakaoonyesha uwezo mkubwa na kiwango kizuri katika mashindano haya wataitwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa kwa ajili ya maandalizi ya kushiriki Mashindano ya Ubingwa wa Afrika yatakayofanyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mwezi Oktoba 2026*_ .

Kwa hiyo, mashindano ya mwaka huu yana umuhimu wa kipekee kwa kuwa yanatoa fursa kwa mabondia kuthibitisha uwezo wao na kupata nafasi ya kuwania kuwakilisha taifa katika jukwaa la kimataifa.

Mwaliko kwa wananchi na wadau

Shirikisho la Ngumi Tanzania linawaalika wananchi wa Tanga, mashabiki wa mchezo wa ngumi na wadau wa michezo kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika Viwanja vya Mkwakwani leo kuanzia saa 10:00 jioni, kushuhudia ushindani wa mabondia kutoka vilabu mbalimbali nchini.

Mashindano haya ni sehemu ya juhudi za kuimarisha mchezo wa ngumi nchini, kutoa nafasi kwa vipaji vipya na kuandaa mabondia wenye uwezo wa kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kikanda, bara na kimataifa.

Klabu Bingwa Taifa 2026 — Tanga

Mahali: Viwanja vya Mkwakwani, Tanga

Tarehe:25 Agosti 2026

Muda: Saa 10:00 jioni

Makore Mashaga

Katibu Mkuu

Shirikisho la Ngumi Tanzania
 

0/Post a Comment/Comments