MAIMAMU NA WALIMU WA MADRASA WAWEZESHWA KUJIKWAMUA KIUCHUMI


 ******

Maimamu na walimu wa madrasa nchini wamepewa vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kuboresha maisha yao.

Uwezeshaji huo umetolewa na Umoja wa Maimamu na Walimu wa Madrasa Tanzania (UMATA), kwa kushirikiana na taasisi ya Humanity Without Borders kutoka Uingereza.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kitaifa wa UMATA, Sheikh Arif Surya, amesema baadhi ya maimamu wamepewa friji kwa ajili ya biashara ya juisi na maji.

Amesema wengine wamepatiwa vifaa vya kuanzisha biashara ndogondogo, ikiwemo biashara ya dawa za asili, huku wakulima wakipewa pampu na vifaa vya umwagiliaji.

Sheikh Surya amesema UMATA inaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali ndani na nje ya Tanzania katika kuwawezesha maimamu na walimu wa madrasa.

Amesema kuwawezesha maimamu ni muhimu kutokana na nafasi yao katika kuwaongoza waumini katika ibada, malezi na maendeleo ya jamii.














0/Post a Comment/Comments