MHARIRI STAR TV AIBUKA MSHINDI TUZO ZA AFYA ZA TAMDA

.........

Mhariri wa Maudhui Mtandaoni katika Kituo Cha Runinga Cha Star Tv, Caren-Tausi Mbowe ameibuka mshindi katika uandishi wa habari za Afya  zinazohusu Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi.

Tuzo hizo zinazotolewa na Mamlaa ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA ), zimetolewa mjini Babati mkoani Manyara katika kikao kazi baina ya mamlaka hayo na wahariri na waandishi wa habari wa Kanda ya Kaskazini ikijumulisha mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara.

Katika tuzo hizo, Caren-Tausi ameibuka mshindi wa kwanza katika kundi la runinga na kukabidhiwa cheti, ngao na fedha taslimu.

Washindi wengine ni Aveline Kitomari wa Habari leo na Daily News ameishinda kwa upande wa Magazeti, John Bukuku wa  Full Shangwe ameshinda upande wa Digital na Agatha Kisimba wa Radio Maria akinyakua ushindi Kwa upande wa Radio





 

0/Post a Comment/Comments