MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA KIBAHA AZINDUA MAGARI KWA AJILI YA MRADI WA TACTIC

.....

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dkt Nicas Mawazo amepokea na kuzindua magari mawili ya Ford Ranger kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa Tactic na kuahidi kuwa Manispaa ya Kibaha inaenda kuwa namba moja kitaifa kwenye usimamizi wa mradi huo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa magari hayo, Dkt Nicas amesema anaishukuru serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta mradi mkubwa wenye thamani ya Bilioni 19.8 unaoenda kuleta mabadiliko chanya na uboreshaji wa miundo mbinj mbalimbali ya Manispaa ya Kibaha.

Dkt Nicas amesema magari haya ni moja ya makubaliano mkataba wa mradi huo kuna magari ambapo yakimaliza kutumika yanarudi Halmashauri kwa ajili ya shughuli zingine.

Amesema, katika miradi hii ya Tactic wanakwenda kuitekeleza kwa ubora zaidi na Halmashauri ya Kibaha inaenda kuwa ya kwanza na mfano kwa Halmashauri zingine katika utekelezaji na usimamizi wa miradi hii nchini.

Dkt Nicas amewataka wananchi wa Kibaha kujivunia na kutangaza maendeleo yanayofanywa na serikali hii, kwani Manispaa ya Kibaha ina neemeka na dira ya Mhe Rais na mmeona maendeleo yanavyokuja kwa kasi na tutakuwa halmashauri ya mfano kwa kila kitu.

Akisoma taarifa ya mradi huo, Afisa Utumishi Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Mrisho Mlelaamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta miradi yenye fedha nyingi sambamba na Mkuu wa Mkoa Mhe. Abuubakari Kunenge na Mkuu wa Wilaya Mhe Nickson Simon John kwa usimamizi mzuri na utekelezaji wa Ilani kwa maslahi ya Manispaa ya Kibaha.

Aidha, amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dkt Rogers Shemwelekwa kwa usimamizi mzuri wa masuala mbalimbali ya mapato, usimamizi wa miradi pamoja na tija katika utendaji wa Halmashauri.

Halmashauri ya Manispaa imepokea magari hayo mawili kutoka kwenye Mkataba wa mradi wa Tactic ambapo yatatumika katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Tughe -Angulcan , barabara ya Picha ya ndege - Lulanzi, soko la mnarani.

 

0/Post a Comment/Comments