OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAWASILISHA MAJIBU KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA MBALIMBALI NA. 2 WA MWAKA 2026


 *****

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imewasilisha majibu ya Serikali kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 2 wa Mwaka 2026 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria.

Majibu hayo yamewasilishwa leo, Agosti 18, 2026, katika shughuli za Bunge jijini Dodoma, huku Serikali ikitoa ufafanuzi kuhusu mapendekezo yaliyomo kwenye Muswada huo.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari, ameongoza jopo la wataalamu wa sheria katika kuwasilisha majibu ya Serikali mbele ya Kamati hiyo.

Akizungumza kuhusu Muswada huo, Mwandishi Mkuu wa Sheria, Bw. Onorius Njole, ametaja baadhi ya sheria zinazokusudiwa kufanyiwa marekebisho.

Sheria hizo ni pamoja na Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori Sura ya 283, Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287, Sheria ya Utathmini na Usajili wa Wathamini Sura ya 138, Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura ya 288 pamoja na Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Sura ya 116.







0/Post a Comment/Comments