Kwa vijana wengi wanaopenda kujaribu vitu vipya, ORIJIN imekuwa sehemu ya mazungumzo katika siku za hivi karibuni. Baada ya kuzinduliwa rasmi nchini, bidhaa hiyo imeendelea kuvutia watu wanaotafuta ladha tofauti na walizozoea.
Ladha yake inayochanganya uchungu na utamu imekuwa sababu kubwa ya watu kuwa na maoni yanayotofautiana. Wengine wanaiona kama uzoefu mpya, huku wengine wakisema imeleta kumbukumbu za ladha za asili za Kiafrika.
Mijadala hiyo imeendelea kuonekana kwenye maeneo ya burudani, ambapo marafiki hukutana na kubadilishana maoni kuhusu bidhaa mpya wanazozijaribu. Hali hiyo imeifanya ORIJIN kuendelea kutajwa mara kwa mara.
Kwa sasa, ORIJIN inapatikana katika ORIJIN Bitters na ORIJIN Mixed (RTD), ikiwa na bei zinazowapa watumiaji nafasi ya kuchagua kulingana na mapendeleo yao.
Kadri walaji wanavyoendelea kuifahamu, ndivyo mazungumzo yanavyozidi kuongezeka, jambo linaloifanya ORIJIN kuendelea kuwa moja ya bidhaa zinazovutia umakini wa wengi.






Post a Comment