Askofu Msaidizi Mteule jimbo Kuu la Dar es salaam Padre Vincent Mpwaji akizungumza katika halfa ya kuwapongeza na kumshukuru Mungu kwa zawadi ya Mapadri wapya ambayo imeratibiwa na Jumuiya ya Wazazi na walezi wa mafrateri (JUWAMA) na kufanyika katika Kanisa la Parokia ya Mashidi wa Uganda Magomeni.
Paroko wa Parokia ya Magomeni Padre Benno Kiduko akizungumza katika halfa ya kuwapongeza na kumshukuru Mungu kwa zawadi ya Mapadri wapya ambayo imeratibiwa na Jumuiya ya Wazazi na walezi wa mafrateri (JUWAMA) na kufanyika katika Kanisa la Parokia ya Mashidi wa Uganda Magomeni. (Picha na Mussa Khalid)
...............
NA MUSSA KHALID
Mapadri wapya 18 wametakiwa kuwa waaminifu kwa kujitoa kwa ajili ya kanisa na Mungu ili waweze kuwahudumia watanzania na taifa liendelee kuwa na amani wakati wote.
Hayo yamejiri jijini Dar es salaam katika halfa ya kuwapongeza na kumshukuru Mungu kwa zawadi ya Mapadri hao ambayo imeratibiwa na Jumuiya ya Wazazi na walezi wa mafrateri (JUWAMA) na kufanyika katika Kanisa la Parokia ya Mashidi wa Uganda Magomeni.
Akizungumza wakati akiongoza Misa takatibu iliyofanyika katika kanisa hilo Askofu Msaidizi Mteule jimbo Kuu la Dar es salaam Padre Vincent Mpwaji amewapongeza kwa kufanikiwa kwa hatua kukwepa vikwanzo na viunzi ambavyo vinawazuia kufika malengo.
Kwa upande wake Paroko wa Parokia ya Magomeni Padre Benno Kiduko amewasisitiza wazazi na walezi kuendea kuwasindikiza na kuwalea mafrateri na sio kuiachia kanisa pekee.
Mkurugenzi wa Miito Jimbo kuu la Dar es salaam Father Denis Ngumba ambaye pia ni Mlezi wa Jumuiya ya Wazazi na walezi wa mafrateri (JUWAMA) amesema hafla ya leo ni muendelezo ambapo kila Agost 8 ya kila mwaka ambapo wanakuwa na mapadri wapya kutoka katika Jumuiya hiyo wakimshukuru Mungu.
Nao wawakilishi wa mapadri wapya ambao wamepata pongezi akiwemo Father Emmanuel Shaaban Ibrahim na Father Inyasi Mansweti Maresi ambao ni Mapadri kutoka jimbo kuu Dar es salaam na Mwalimu na Mlezi Seminari Ndogo ya Visiga wamesema kilichowavutia kutaka kuwa Padri ni kwa lengo la kutaka kutoa huduma.
Mapadri wengine waliopongezwa ni pamoja na Hinky Perez De la Rosa,Alex Benward Mlaponi,George Ngisaise,Godfrey Pascal Mallya,Inyasi Maresi,Noel Levaria,Petro Augustino Tarmo,na Benson Andrew Mpangala
Post a Comment