Na Ester Maile TANGA
MRADI wa TarL unaotekelezwa na kampuni ya Innovet Foundation chini ya program ya TangaYetu umeweza kubaini watoto 4200 waliokuwa hawajui Kusoma,Kuandika na Kuhesabu na kusaidiwa ili kuwa na uelewa stahiki.
Mratibu wa TarL katika Halmashauri yabTanga Alex Sijalla amesema hayo wakati akizungumza katika wiki ya elimu ujuzi na ubunifu 2026 inayoendelea katika viwanja vya usagara na kuongeza kuwa mbinu ya TarL inawasaidia watoto wenye changamoto na kuhakikisha wanazimudu.
Amesema katika banda la TangaYetu wanaonesha michezo na mbinu mbalimbali zinazoweza kutumiwa na walimu ili mtoto aweze kumudu Kusoma,Kuandika na Kuhesabu katika ngazi husika.
Aidha amesema kwa mbinu hiyo mradibumetoa mafunzo kwa walimu 176 nan kwenye ngazi ya kata kuna ofisa elimu kata ambao wanasaidia kusimamia waroro kwenye ngazi hio na kwenge halmashauri kuna wadhibiti ubora wanaosaidia kufuatilia watoto kujia Kusoma kuandika na kuhesabu.
Anawakaribisha wananchi kufika katika banda hilo ili kujifunza mbinu mbalimbali.
Ofisa Mradi Msaidizi wa Program ya Tanga Yetu Hadija Idrisa amesema program inafadhiliwa na shirikabla Kiswizi la Foundation Botter kwa kushirikiana na Halmashauri ya Tanga ikisimamiwa na Innovet Development Consult Ltd.
Amesema lengo ni kusaidia kuboresha ustawi na afya ya vijana na watoto wa Tanga na ina maeneo sita ya kipaumbele ikiwemo afya,elimi,ubunifu,teknolojia, mazingira,ushirikishwaji jamii na uwezeshaji kiuchumi.
Amesema katika wiki ya elimu,ujuzi na ubunifu wadau mbalimbali wanaonesha kuhusu mradi na kuwakaribisha wananchi kushiriki na kujifunza.
Kwa upande wake Mkufunzi wa mbinunya TarL Batuli Msuya amesema ni mbinu inayomfanya mtoto kugusa kucheza kuimba na kufurahi nankuwasihi walimu kuitumia kwa lengo la kusaidia watoto.


Post a Comment