RC CHALAMILA ATOA AGIZO KWA TANROADS DAR KUKAMATA MALOLI YOTE BARABARA MANDELA

Mkuu wa mkoa Dar es Salaam Albert John Chalamila, akizungumza na wananchi wa Tuangoma katika ziara yake Wilayani Temeke leo katika ziara hiyo yenye dhumuni la kutatua kero na kuangalia miradi ys Serikali (PICHA NA HERI SHAABAN)

............

Na Heri Shaaban (Dar es Salaam)

MKUU wa Mkoa Dar es Salaam Albert Chalamila, ametoa agizo kwa Wakala wa Barabara nchini TANROADS kuanzia leo kukamata Maloli yote ya mizigo barabara ya mandela katika barabara ya Watembea kwa miguu.

Mkuu wa mkoa Albert Chalamila, alitoa agizo hilo Dar es Salaam leo,katika ziara yake ya kutatua kero wilaya ya Temeke Mkoa Dar es Salaam. 

"Natoa agizo kwa Wakala wa Barabara TANROADS kuanzia leo kukamata maloli yote ya mizigo ya makontena yanayopaki katika barabara za Watembea kwa miguu katika barabara hii ya mandela imekuwa kero kubwa pamoja na mabasi marufuku kupaki katika hifadhi ya barabara "amesema Chalamila  

Chalamila amesema kuanzia leo Dereva yoyote atakayepaki loli katika barabara hiyo akamatwe kwani kufanya hivyo ni kujichukulia sheria mkononi wakati wakijua ni kosa kisheria.

Alitoa onyo kwa mamlaka husika ambayo inatoa vibari vya maloli ya makontena ambayo yanapaki barabarani wasitoe vibari ovyo kula pesa zingine za moto na maloli yakitaka kupaki yafuate taratibu za vibari mamlaka husika. 

Wakati huo huo alitoa agizo kwa Bandari kavu zote Wilaya ya Temeke ICD kukutana katika cha zarula siku ya Jumatano asubuhi kwa ajili ya kutatua changamoto za kupaki ovyo barabara ya Sandali kutokea Mchicha. 

Katika hatua nyingine akizungumzia barabara ya Tuangoma alipongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kujenga Barabara hiyo ya viwango kwa viwango vya zege kwani miundombinu ya zege inadumu sana .

Aliwataka wananchi wa Wilaya ya Temeke mkoa Dar es Salaam kudumisha amani kwani amani ni tunu ya Taifa letu Tanzania  

Mwisho


 

0/Post a Comment/Comments