SEIF GULAMALI KIELELEZO CHA UONGOZI NA HEKIMA

....

Seif Gulamali: 

Kielelezo cha Uongozi wa Hekima na Upendo kwa Jamii

Aliiongoza Manonga kwa Weledi Mkubwa

 'Figisu' Ujumbe Kamati Utendaji Yanga wamtoa uongozini

KATIKA Jamii yoyote, viongozi bora ni wale wanaotambua kwamba mafanikio ya kweli hupimwa kwa mchango wao katika kuboresha maisha ya wengine kwa namna moja au nyingine.

Miongoni mwa watu wanaotajwa kwa sifa nzuri za uongozi unaojengwa juu ya maadili, uwajibikaji na upendo kwa jamii ni pamoja na Seif Gulamali, kijana mpole ambaye amewahi kuliongoza Jimbo la Manonga kwa kipindi Cha awamu mbili tofauti, akitimiza majukumu yake ya kuwatumikia wananchi.

Kwa wasiomfahamu Gulamali, sifa yake kubwa ni uwezo wa kuwasikiliza watu na kuthamini mawazo yao bila ubaguzi wa aina yoyote na zaidi akiwa kiongozi aliyejijengea tabia ya kuwa msikilizaji wa masuala mbalimbali ya kijamii na hasa yale yanayogusa maisha ya watu.

Kupitia mwenendo wake, Seif Gulamali ameonyesha kuwa uongozi si mamlaka pekee, bali ni huduma kwa watu na kujitoa kwa ajili ya manufaa ya wengi pasipo kuwabagua kwa namna moja au nyingine kutokana na hali zao au nafasi zao za uongozi.

Aidha, anajulikana kwa kuamini katika mshikamano na ushirikiano akiendelea kuhamasisha watu kufanya kazi pamoja sambamba na kutatua changamoto kwa mazungumzo na kujenga umoja unaowezesha jamii kusonga mbele.

Upendo wake kwa jamii unaonekana katika namna anavyowathamini watu wa rika na makundi mbalimbali akitambua kuwa kila mtu ana nafasi ya kuchangia maendeleo, hivyo huwahimiza vijana kutumia vipaji vyao, huku akiheshimu mchango wa wazee na wanawake katika kujenga taifa lenye mshikamano.

Pia, Seif Gulamali ni mfano mzuri wa mtu anayesisitiza maadili, uadilifu na heshima kuwa ni moja ya uwajibikaji, hizi ni sehemu muhimu miongoni mwa sifa za uongozi unaodumu na unaoleta matokeo chanya kwa jamii akiamini kutenda haki hujenga imani kwa wananchi na kuimarisha ushirikiano katika kufikia malengo ya pamoja.

Akiwa Mbunge kwa wananchi wa Jimbo la Manonga,Seif Gulamali anaweza kutazamwa kama mfano wa uongozi unaozingatia utu, mshikamano na upendo kwa jamii, akishiriki katika masuala mbalimbali ya Kimaendeleo ulioliwezesha Manonga kupiga hatua.

Wakati wa Ubunge wake, Seif Gulamali ambaye ni Mwanachama Kindakindaki wa Klabu ya Yanga, pia amewahi kushika nafasi ya kuwa Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, akifanikiwa kuifanya timu hiyo ya Wananchi kupiga hatua kubwa na Muhimu ikiwemo kubeba nakuomba mbalimbali likiwemo la Ligi Kuu ambapo kwa msimu ulioisha imelibeba Taji hilo kwa mara ya 5 mfululizo.

Ameonyesha kuwa uongozi si nafasi ya kujinufaisha binafsi, bali ni dhamana ya kuhakikisha taasisi inapata maendeleo endelevu, sifa hizi ndizo zilizomfanya aonekane kuwa mmoja wa watu wanaoweza kutoa mchango mkubwa katika kuendelea kuijenga Yanga.

Pamoja na kutofanikiwa kupenya katika nafasi nne za Kamati ya Utendaji Yanga kwa madai ya uwepo wa Figisu licha ya jina lake kushika nafasi ya tatu, Gulamali ameendelea kuamini kuwa Yanga inaweza kufikia mafanikio makubwa zaidi ikiwa kutakuwa na ushirikiano, uwajibikaji na usimamizi makini wa rasilimali za klabu sambamba na umoja kutoka kwa kila Mwanachama.

Kimsingi mtazamo huu ni dhahiri kuwa unaonyesha dhamira yake ya kuona Yanga ikiendelea kuwa kinara ndani na nje ya Tanzania na kuziacha timu zingine zikiwa kama wasindikizaji katika malengo iliyojiwekea.

Aidha, Gulamali ni miongoni mwa viongozi ambao wamekuwa wakionesha mapenzi ya dhati kwa Yanga kwa muda mrefu huku ikiaminika kuwa Mapenzi yake ya kweli kwa klabu ni kuitumikia kwa moyo wote na kuhakikisha maslahi ya klabu yanatangulizwa mbele ya maslahi binafsi. 

Kwa miaka ya hivi karibuni, Gulamali amekuwa akitajwa miongoni mwa viongozi wanaoshiriki katika maendeleo ya Yanga na amewahi kueleza dhamira yake ya kusaidia kuisimamia klabu na kuendeleza mabadiliko ndani ya Yanga. Pia amewahi kuwa sehemu ya uongozi wa klabu hiyo kama mjumbe wa Kamati ya Utendaji, akichangia safari ya maendeleo ya Wanajangwani.

Wahenga Wana Usemi Usemao " Safari ni hatua" Yes na Kila jambo lina wakati wake, hatua ya kutopewa nafasi katika Kamati hiyo ya Utendaji Yanga, ukaribu wake na Kila mtu unatoa nafasi nyingi kwa Mwana Manonga kuendelea na hatua nyingine ingawa haina maana kuwa nafasi yake ya kuwatumikia wananchi ( Yanga) imefikia tamati.

Kwa wale tunaomtambua tunasema "Songa mbele" Mwamba Wananchi wa Manonga bado wanakuhitaji, "Songa mbele" Mwamba Wananchi wa Jangwani bado wanakutegemea"

Mwisho

 

0/Post a Comment/Comments