

Mwenyekiti Mpya wa TPF
Wilaya ya Temeke William Odingo Gereshon akizungumza katika kikao cha wajumbe
wa Taasisi hiyo sambamba na utambulisho wa Viongozi wapya wa Wilaya ya Temeke
ambacho kimefanyika tar 1/8/2026 jijini Dar es salaam.

.....................
Taasisi ya Tanzania Peace Family (TPF) Mkoa wa Dar es salaam imewasisitiza viongozi na wajumbe wa Taasisi hiyo Wilaya ya Temeke kuhakikisha wanaendelea kudumisha na kuhamasisha umoja na amani ili kuenzi tunu iliyoacha na waasisi wa taifa hili.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Kiongozi wa Itifaki na usalama Mkoa wa Dar es salaam Ediga Ishemujabi wakati akizungumza katika kikao cha wajumbe wa Taasisi hiyo sambamba na utambulisho wa Viongozi wapya wa Wilaya ya Temeke.
Ishemujabi amewasisitiza Viongozi waliopata nafasi ya kuteuliwa leo kwenda kufanya kazi ya kuisemea amani ya nchi kwa ueledi ili taifa liendelee kuwa imara wakati wote.
Aidha amewasisitiza viongozi hao kuhakikisha wanazingatia kanuni ya P5 kwani itawawezesha kuitangaza amani vyema pasipo changamoto kutoka kwa watu jambo litakalowasaidia kuwa na uongozi imara.
Awali Akizungumza katika Kikao hicho Katibu Mkuu wa Taasisi ya Tanzania Peace Family (TPF) Mkoa wa Dar es salaam Elizabeth Sheyo ametumia fursa kuwakumbusha wajumbe na Viongozi kutekeleza wajibu wao kwa kufata miongozo ya taasisi hiyo.
Amewasisitiza kuhakikisha wanaheshimiana katika nafasi zao kwani jambo la kuisemea amani ya nchi linaanza kuanzia katika ngazi za chini.
Pia amesisitiza suala la kuendelea kuongeza wanachama wapya na waadilifu watakaojumuika kwa pamoja katika kuihamasisha amani ya nchi kwenye jamii zao.
Akizungumza baada ya kuteuliwa Mwenyekiti Mpya wa TPF Wilaya ya Temeke William Odingo Gereshon pamoja na viongozi wengine waliotangazwa kwa umoja wao wamesema watahakikisha wanafanya kazi ya kuihamasisha amani kwa juhudi na bidii ili kuendelea kuijenga nchi.




Post a Comment