Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatarajia kufunga Scanner kwaajili ya ukaguzi wa mizigo kwenye Bandari ya Mkoani Kisiwani Pemba Ili kuongeza ufanisi na kutanua wigo wa huduma katika Bandari hiyo.
Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda akiwa ziarani Kisiwani Pemba amesema kufungwa Kwa Scanner kwenye Bandari ya Mkoani kutaendelea kuboresha zaidi huduma kwa Wananchi wanaotumia Bandari hiyo na kuongeza mapato ya kodi yatakayoenda kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi.
Amesema lengo la TRA ni kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi na kuhamikisha kila mmoja analipa Kodi stahiki na kila anayetakiwa kulipa Kodi analipa Kodi kwa maendeleo ya Taifa.
"Scanner itakayofungwa hapa bandarini itasaidia kudhibiti bidhaa zinazoingizwa Kwa magendo ambazo zimekuwa zikikwepa Kodi na kuingima Serikali Mapato lakini pia itasaidia kuzuia bidhaa zisizoruhusiwa kuingia nchini ambazo Zina madhara Kwa Wananchi.
Katika hatua nyingine Mwenda amesema TRA inaendelea na hatua za kujenga Ghala la Forodha (Bonded Warehouse) katika eneo la Mkoani hali ambayo itaongeza wingi na usalama zaidi wa shehena zinazopitia bandarini hapo.
Kwa upande wake msimamizi wa Kituo Cha Forodha kwenye Bandari ya Mkoani Bw. Abdallah Salim Abdallah amesema ujenzi wa Ghala la Forodha katika Bandari hiyo utabiresha zaidi utoaji wa huduma kwa wananchi katika Bandari hiyo na kuiongezea Serikali mapato.
Amesema Bandari ya Mkoani ni ya pili Kwa ukubwa Visiwani humo na imekuwa ikipokea Meli kubwa za mizigo kutoka maeneo mbalimbali na hivyo kuchangamsha uchumi wa Kisiwa cha Pemba.
========



Post a Comment