WAGANGA WA JADI WAPEWA ELIMU JUU YA KUFANYA KAZI ZAO BILA KUVUNJA SHERIA


.....

Na Ester Maile Dodoma 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gallus Hyera amewapeleka Waganga wa Jadi wa Mkoa huo kwenye Maonesho ya wakulima Nanenane ilikuwapa Elimu ya kutekeleza majukumu yao kwa kufuata sheria, nakuwasihi wawafichua waalifu wanaofika kwao baada ya kutekeleza makosa mbalimbali nakuwahimiza waache kufanya ramli chonganishi

Kamanda wa Polisi Gallus Hyiera, amesema hayo leo Jijini Dodoma, baada ya kumalizika kwa maandamano yaliyohusisha Jeshi hilo na Chama cha Waganga wa Jadi wa Mkoa huo pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi na Sekondari, katika viwanja vya Nanenane kwa lengo la kutoa elimu juu ya utii wa sheria bila shuruti lakini pia kutoa elimu kwa waganga hao ili watekeleze majukumu yao bila kuvunja sheria.

0/Post a Comment/Comments