...........
Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi (Mb.), amewasili mkoani Shinyanga kwa ziara maalum ya kikazi ya kukagua utekelezaji na kuzindua miradi ya maendeleo, pamoja na kuzungumza na wananchi katika wilaya za Mkoa wa Shinyanga.
Waziri Ndejembi, ambaye ni Mlezi wa Mkoa wa Shinyanga Kiserikali, mara baada ya kuwasili amefika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Mboni Mhita, tarehe 09 Agosti 2026.








Post a Comment