********
Mjumbe Maalumu wa Masuala ya wanawake Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika (AU), Balozi Liberata Mulamula, ametoa salama za pole kwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha Mwenza wake, Mzee Hafidh Ameri.
Akielezea kuhusu taarifa ya Msiba huo, amesema ameipokea kwa mshtuko mkubwa, kwa vile alivyo mfahamu wakati wa uhai wake, akiwa ni Mzee Mnyenyekevu.
"Nimepokea taarifa za msiba kwa masikitiko makubwa, Ni taarifa ya kusikitisha sana. Binafsi nilimfahamu Mzee Hafidh Ameri, katika ziara mbali mbali za uongozi. Alikuwa mwema na mnyenyekevu sana. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.
"Natoa pole sana kwa Mheshimiwa Rais Dk.Samia, kwa kuondokewa na mpendwa wake, naendelea kumuombea faraja na moyo wa subra katika kipindi hiki kigumu,"amesema Balozi Liberata Mulamula

Post a Comment