DAR ES SALAAM, Septemba 3, 2026
Jumla ya kazi 294 zimefuzu kuingia hatua ya kupigiwa kura na wananchi katika msimu wa pili wa Tuzo za Samia Kalamu Awards (SKA 2026).
Kazi hizo zimechaguliwa kutoka kazi 3,003 zilizowasilishwa na waombaji 985, baada ya kutathminiwa kwa kuzingatia ubora, ubunifu, utafiti, maadili ya taaluma na athari kwa jamii.
Akizungumza leo, Mwenyekiti wa Maandalizi ya Tuzo hizo, ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mha. Peter Mwasalyanda, amewataka wananchi kushiriki kupiga kura.
Amesema kura zinaweza kupigwa kupitia tovuti ya tuzo au kwa kutuma ujumbe wenye neno “SKA” likifuatiwa na namba ya mshiriki kwenda 15200. Zoezi limeanza leo na litafungwa Septemba 30, 2026.
Mwenyekiti Mwenza wa Mashindano hayo na Mkurugenzi wa TAMWA, Dkt. Rose Reuben, amesema tuzo hizo zimewakutanisha waandishi kutoka vijijini na mijini, huku akisisitiza ushindani kuzingatia ubora wa kazi, si umaarufu.
Kwa upande wake, mmoja wa majaji, Bi. Beatrice Bandawe, amesema kazi zilizowasilishwa zimegusa maeneo mbalimbali, ikiwamo afya, jinsia na makundi maalum, mazingira pamoja na elimu.









Post a Comment