......
Mfanyabiashara wa Zimbabwe, Wicknell Chivayo, pamoja na mke wake Lucy “Lulu” Muteke, wamefariki dunia Jumatano jioni baada ya helikopta waliyokuwa wakisafiria kuanguka katika eneo la Marondera Rural, mashariki mwa Harare.
Polisi wa Zimbabwe walithibitisha ajali hiyo ya ndege iliyotokea majira ya saa 11:00 jioni, wakisema awali kulikuwa na watu sita ndani ya helikopta hiyo. Polisi walisema taarifa zaidi zitatolewa wakati uchunguzi ukiendelea.
Baadaye, msemaji wa serikali Nick Mangwana alithibitisha kuwa hakukuwa na manusura.
Alisema watu saba walikuwa ndani ya helikopta hiyo, akiwemo Chivayo, abiria wengine wanne na marubani wawili. Mamlaka bado hazijabaini chanzo cha ajali hiyo



Post a Comment