Uongozi wa Young Africans Sports Club umetangaza kifo cha Mwanachama wake, Haji Omari Ramadhani Mpili, kilichotokea usiku wa Septemba 27, 2026 katika Kituo cha Afya cha Wilaya ya Ikwiriri, mkoani Pwani alipokuwa akipatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga leo Septemba 28, 2026, mazishi ya Marehemu yanatarajiwa kufanyika kesho majira ya saa 10 jioni katika Makaburi ya Msikiti Mkuu, Wilaya ya Ikwiriri, mkoani Pwani.
Uongozi wa Yanga umetoa pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa, Marafiki pamoja na Wadau wote wa mpira na kuwaomba kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu.
“Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amina

Post a Comment