NAIBU WAZIRI CHANDE ASHIRIKI ZOEZI LA KUZIMA MOTO KINAPA*

...........

Na Mwandishi wetu, Kilimanjaro 

Leo tarehe 29 Septemba, 2026 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) amefika eneo la Hifadhi ya Taifa Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kushiriki na kusimamia zoezi la kuzima moto kwenye eneo la Shira 1 na Shira 2 lililopo Mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza na wananchi na vikosi vya kuzima moto katika eneo hilo,  Mhe. Chande amewatia moyo na kubainisha kuwa Serikali ipo pamoja nao katika kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na majanga ya moto kuepuka kuleta madhara pindi yanapotokea majanga kama hayo na kuepuka kuharibu uoto wa asili uliopo  kwenye maeneo ya hifadhi yenye umuhimu mkubwa katika shughuli za kitalii na uhifadhi.

Aidha, Mhe. Chande amepongeza  Jeshi la Uhifadhi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na wananchi katika kukabiliana na moto huo na kufanikiwa kuudhibiti  kutosambaa katika maeneo mengine kuharibu uoto wa asili wa eneo ya hilo huku akiwatoa hofu wananchi wanaoishi maeneo ya jirani

"Niwatoe hofu wananchi wenzangu kwamba, kwa juhudi na nguvu ambayo imetumika kwa askari wetu namna ya kupambana na moto huu, mapema tutafanikiwa  kudhibiti, kutokana na ufanisi wa vikosi vyetu vya uhifadhi na Zimamoto. Amesema Mhe. Chande

Katika hatua nyingine Mhe. Chande amewataka wananchi hayo kuwa watulivu na hakuna hatari yoyote itakayowakuta huku akithibitisha usalama wa askari wanaokabiliana na moto huo na wageni wanaotembelea kwenye maeneo mengine ya hifadhi hiyo wakiwa salama na uangalizi mkubwa wa wahifadhi na kusisitiza kuwa serikali itaongeza nguvu zaidi ya kupeleka askari kwa ajili ya kukabiliana na moto huo kwa haraka zaidi

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe. Dkt. Christopher Timbuka amepongeza hatua za haraka zilizochukuliwa na Wizara kupitia jeshi la uhifadhi katika kupambana na matukio ya moto yanayozuka msituni huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kukabiliana na matukio ya moto kwenye  hifadhi.








0/Post a Comment/Comments