REA YATOA SALAMU ZA POLE KUFUATIA KIFO CHA MFALME HARALD V WA NORWAY


 ...

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mha. Hassan Saidy, amewaongoza Watumishi wa Wakala kutoa salamu za pole na rambirambi kufuatia kifo cha Mfalme Harald V wa nchini Norway.

Mha. Saidy, akiwa ameambatana na Watumishi wa REA, walifika katika Makazi ya Balozi wa Norway nchini Tanzania, ambapo walipokelewa na Balozi wa Norway nchini, Mhe. Tone Tinnes, na kupata fursa ya kuwasilisha salamu za rambirambi kwa niaba ya Bodi, Menejimenti na Watumishi wa Wakala wa Nishati Vijijini.

Katika salamu hizo, REA imeeleza masikitiko yake kufuatia msiba huo na kuungana na Familia ya Kifalme, Serikali pamoja na wananchi wa Norway katika kipindi hiki cha maombolezo, huku ikiwatakia moyo wa subira na faraja wakati huu wa kuondokewa na kiongozi wao.

Ziara hiyo pia ni ishara ya mshikamano na uhusiano mwema uliopo kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia REA na Serikali ya Norway ikiwa ni Mshirika wa Maendeleo katika kuunga mkono juhudi mbalimbali za maendeleo ya sekta ya nishati nchini Tanzania

Zifuatazo ni baadhi ya picha za Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mha. Hassan Saidy, pamoja na Watumishi walipofika kutoa salamu za pole na rambirambi.

0/Post a Comment/Comments