TCB, MDHAMINI MKUU WA C-CEOs FORUM 2026 - KASI KUELEKEA DIRA 2050

*******

Benki ya Biashara Tanzania (TCB), ikiwa Mdhamini Mkuu wa C-CEOs Forum kwa mwaka wa tatu mfululizo, imeshiriki Jukwaa hilo lililolenga kuimarisha utendaji wa Taasisi na Mashirika ya Umma na kuongeza mchango wao katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Katika Jukwaa hilo, TCB imeonesha hatua inazochukua katika kujiimarisha kama taasisi ya fedha yenye uwezo wa kuchochea uwekezaji, uzalishaji na ukuaji wa uchumi, ikiwemo kuendelea kuongeza faida na mikopo mwaka hadi mwaka.

Sambamba na hilo, TCB inaendelea kujiandaa kuingia katika soko la mitaji, ikiwa ni sehemu ya safari ya kujenga taasisi imara, yenye ushindani na inayoweza kutoa fursa zaidi za ushiriki wa Watanzania katika umiliki wa Benki yao. Hatua hii inafuatia nia iliyotangazwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina ya kuingiza baadhi ya taasisi zake katika soko la mitaji.

Kwa msingi huu, TCB inalenga kutumia uwezo wake wa kifedha na kidijitali kuchangia katika utekelezaji wa Dira 2050 kwa kukuza uchumi imara, jumuishi na shindani; kuongeza uwekezaji na uzalishaji; pamoja na kupanua fursa za kiuchumi kwa Watanzania.

TCB imejipambanua mbele ya viongozi na wadau wa sekta ya umma na binafsi kama taasisi inayotayari kuongeza kasi, kuendeleza ubunifu na kutumia nguvu yake ya kifedha na kidijitali kuchangia kwa vitendo katika safari ya Tanzania kuelekea Dira 2050.






#TCB #CCEOsForum2026 #Dira2050 #BenkiInayomwelewaMtanzania
 

0/Post a Comment/Comments