Maafisa wa Taasisi ya Tanzania Peace Family (TPF) mkoa wa Dar es salaam wakiwa katika picha ya pamoja katika uzinduzi wa kitabu cha Amani kilichoandikwa na Bi. Jailya Katende, kwenye hafla ambayo imefanyika tar 20 Septemba katika viwanja vya Mwembeyanga Manispaa ya Temeke
Baadhi ya maafisa wa Taasisi ya Tanzania Peace Family (TPF) mkoa wa Dar es salaam wakishiriki zoezi la uchangiaji Damu katika uzinduzi wa kitabu cha Amani kilichoandikwa na Bi. Jailya Katende, kwenye hafla ambayo imefanyika tar 20 Septemba katika viwanja vya Mwembeyanga Manispaa ya Temeke
.......
Taasisi ya Tanzania Peace Family (TPF) Mkoa wa Dar es salaam imefanikiwa kuongeza wanachama wapya kumi na tano baada ya kuelimishwa kuhusu lengo mahususi la taasisi hiyo katika kuidumisha amani ya nchi
Hayo yamejiri jijini Dar es salaam wakati Taasisi hiyo iliposhiriki katika uzinduzi wa kitabu cha Amani kilichoandikwa na Bi. Jailya Katende, kwenye hafla ambayo imefanyika katika viwanja vya Mwembeyanga Manispaa ya Temeke.
Akizungumza katika Halfa hiyo Katibu wa Tanzania Peace Family (TPF) mkoa wa Dar es Salaam Bi. Elizabeth Sheyo amesema kuwa kutokana na kitabu hicho kuzungumzia Amani ni mwanga wa maisha, msingi wa maendeleo na umoja wa Dunia.
Aidha Katibu huyo akiwa ameambatana na maafisa mbalimbali wa TPF mkoa wa Dar es salaam ametumia fursa hiyo kueleza na kuisihi jamii kuendelea kudumisha amani kwani ndio tunu ya maisha.
Katika Hatua nyingine Viongozi Hao wa Taasisi ya Tanzania Peace Family Mkoa wa Dar es salaam wameshiriki katika zoezi la kuchangia damu kwa ajili ya kusaidia watu wenye uhitaji wa kuongezewa damu.
Ikumbukwe kuwa Tanzania Peace Family (TPF) ni Taasisi iliyoanzishwa kwa lengo la kuimiza amani, umoja, mshikamano na maadili mema katika jamii ya Tanzania









Post a Comment