UWANJA WA NDEGE WA MSALATO WAFIKA 89% - ENG BESTA

.....

Na Ester Maile Dodoma 

 Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Eng. Mohamed Besta, amesema ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato umefikia 89%.

Amesema hayo leo Septemba 24, 2026 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo.

Eng. Besta amesema awamu ya kwanza inayohusisha miundombinu ya msingi ikiwemo barabara ya kurukia na kutua ndege itakamilika ifikapo Desemba 27, 2026.

Aidha kwa awamu ya pili inayohusisha ujenzi wa majengo muhimu kama jengo la abiria, mnara wa kuongozea ndege na kituo cha Zimamoto ujenzi wake utakamilika ifikapo Desemba 30 mwaka huu.

Kukamilika kwa uwanja huo kunatarajiwa kufungua Dodoma kwa safari za moja kwa moja za kimataifa, kuvutia uwekezaji na kuimarisha hadhi ya jiji hilo kama Makao Makuu ya Serikali.

Eng. Besta ametoa wito kwa Watanzania hususani wakazi wa Dodoma kutumia fursa ya uwanja huo wa kitaifa kukuza uchumi wao na uchumi wa taifa kwa kusafirisha mizigo katika nchi mbalimbali.




 

0/Post a Comment/Comments