BFT: MATOKEO YA LEO NA MAPAMBANO YA TANZANIA KESHO NAIROBI

*****

Nairobi, Kenya | 18 Oktoba 2026

Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) linawataarifu Watanzania kuwa mabondia wote watatu wa Tanzania waliopanda ulingoni leo katika Ubingwa wa Afrika wa Ngumi wamepoteza mapambano yao kama ifuatavyo:

1. Mulenga Ally Abeid alipoteza dhidi ya bondia wa Angola kwa majaji 5–1.

2. Mayosa Abdul Mohamed alipoteza dhidi ya Kasuja Richard wa Uganda kwa TKO.

3. Kalabaheleye Shukuru Yoda alipoteza dhidi ya Mohamed Maoui Mohamed wa Angola kwa majaji 5–0.

BFT inawahimiza mabondia wetu kutokata tamaa, bali kujifunza kutokana na matokeo haya na kuendelea kujiandaa kwa mapambano yajayo.

RATIBA YA MABONDIA WA TANZANIA KESHO

Jumatatu, 19 Oktoba 2026

Kuanzia saa 7:00 mchana

Mabondia watatu wa Tanzania wanatarajiwa kupanda ulingoni:

1. Omari Said Korongo dhidi ya Israel Mbaga (Guinea ya Ikweta) — Flyweight, kilo 50.

2. Mkali Moon Rashidi dhidi ya Umunyehirwe Kenny (Rwanda) — Lightweight, kilo 60.

3. Mtwale Hamisi Waziri dhidi Bernardo Massimino Sander Bernardo (Angola) — Welterweight, kilo 65.

BFT inawaomba Watanzania wote kuwaunga mkono, kuwaombea na kuwatia moyo mabondia wetu wanapoiwakilisha nchi katika mashindano haya. Tukiwa pamoja, tuendelee kuwapa hamasa na kuimarisha ari yao ya kupigania ushindi.

WATANZANIA, TUWAUNGE MKONO MABONDIA WETU! 

TUPEPERUSHE BENDERA YA TANZANIA KWA FAHARI!

Imetolewa na:

Makore Mashaga- Katibu Mkuu

Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT)

 

0/Post a Comment/Comments