CHAMARAUTA YAVUNJA MKATABA NA AB FINISH

Mwenyekiti wa Chama cha Mafundi Rangi na Ujenzi Tanzania (CHAMARAUTA) akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam katika ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho leo tar 19/10/2026 
Katibu wa Itikadi na uenezi wa Chama cha Mafundi Rangi na Ujenzi Tanzania (CHAMARAUTA) akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam katika ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho leo tar 19/10/2026 
Mwenyekiti wa Chama cha Mafundi Rangi na Ujenzi Tanzania (CHAMARAUTA Mkoa wa Dar es salaam Dan Ramadhan Kibwana akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam katika ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho leo tar 19/10/2026 
Christina Basili ambaye ni Mtunza Hazina wa Chama cha Mafundi Rangi na Ujenzi Tanzania (CHAMARAUTA Mkoa wa Dar es salaam Dan Ramadhan Kibwana akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam katika ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho leo tar 19/10/2026 

...........

Chama cha Mafundi Rangi na Ujenzi Tanzania (CHAMARAUTA) wamekubaliana kusitisha mkataba wa mashirikiano na Kampuni ya AB Finish kwa maslahi mapana ya chama hicho.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa CHAMARAUTA Juma Chakusaga amesema wamefikia hatua hiyo kutokana na mapato ya kukiendesha chama hicho kutopatikana kwa ufanisi.

Aidha ametumia fursa hiyo kuyataka makampuni na wawekezaji wa sekta ya ujenzi na wazalishaji nchini kushirikiana na chama hicho ikiwemo kuwekeza katika chama hicho ili kupata nguvu ya pamoja.

Katibu wa Itikadi na uenezi wa CHAMARAUTA John Mhali amesema chama kimejipanga kuendelea na majukumu yake mengine kutokana na hasara waliyokuwa wanaipata katika mkataba na AB Finishin

Kwa upande wao Mwenyekiti wa CHAMARAUTA Mkoa wa Dar es salaam Dan Ramadhan Kibwana pamoja na Christina Basili ambaye ni Mtunza Hazina wa Chama hicho wamepongeza hatua hiyo ya kuvunjwa mkataba kwani ulikuwa ukisababisha changamoto kwa wananchama wao.

Hata hivyo Mafundi Rangi na Ujenzi Tanzania wametakiwa kutumia fursa ya kujiunga katika jukwaa hilo ili kuweza kurahisi utendaji wa kazi zao ikiwemo timu zenye uhakika mzuri utakaosaidia kuzitatua changamoto zote zinazowakabili.


















 

0/Post a Comment/Comments