COPRA YAWAKUTANISHA WADAU KUJADILI SOKO LA VIUNGO KUELEKEA DIRA 2050

............

Na Ester Maile TANGA 

Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) imewaunganisha wadau wa sekta ya kilimo katika kuongeza mnyororo wa thamani wa viungo katika mdahalo uliofanyika mkoani Tanga, ikiwana lengo la kujadili changamoto za uzalishaji, ubora, uchakataji na upatikanaji wa masoko, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Chakula Duniani yanayoendelea kuazimishwa kitaifa jijini Tanga.

Hayo yamezungumzwa Leo 13 Oktoba 2026 na Mkuu wa Kanda ya Kaskazini wa COPRA, Fahamia Selemani, amesisitiza umuhimu wa kuzingatia sera na taratibu za kilimo, ikiwemo matumizi ya vifungashio vinavyokidhi viwango, ili kuongeza thamani ya viungo na kuimarisha ushindani katika masoko.

Mdahalo huo umekutanisha , maafisa ugani, Wakulima wataalamu wa masoko, wawakilishi wa Wizara ya Kilimo, Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Wakala wa Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), pamoja na maafisa kilimo wa halmashauri na Mkoa wa Tanga.

Katika majadiliano hayo, wadau wamejadili changamoto zinazowakabili wakulima na wafanyabiashara wa viungo, ikiwemo upatikanaji wa masoko, ubora wa mazao, gharama za biashara na umuhimu wa kuwaunganisha wakulima na wanunuzi ili kuhakikisha uzalishaji unaendana na mahitaji ya soko.

Mdahalo huo umefanyika chini ya kaulimbiu isemayo “Ubunifu katika Mnyororo wa Thamani wa Viungo kwa Kipato Endelevu, Uchumi Imara na Lishe Bora, Kuelekea Dira ya Taifa ya 2050,” inayolenga kuhamasisha ubunifu na ushirikiano katika kuongeza tija, kipato cha wakulima .


 

0/Post a Comment/Comments