MABONDIA WATATU WA TANZANIA KUPANDA ULINGONI LEO KATIKA MASHINDANO YA NGUMI BARANI AFRIKA


 ********

Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) linawataarifu Watanzania kuwa mabondia wake watatu wanatarajiwa kushiriki mapambano leo kuanzia saa 8:00 mchana katika Mashindano ya Ubingwa wa Afrika ya Ngumi, yanayofanyika Ukumbi wa Ndani wa Kasarani, Nairobi, Kenya.


RATIBA YA MAPAMBANO

1. Ally Abeid Mulenga (Kilo 70), Tanzania dhidi ya Joao Umba Luzolo, Angola 

2. Abdul Mohamed Mayosa (Kilo 80), Tanzania dhidi ya Richard Kasuja, Uganda 

3. Shukuru Yodam Kalabaheleleye (Kilo 85), Tanzania dhidi ya Moises Chiangulula Gimbi Fiquissa, Angola.


Shirikisho la ngumi la Taifa linawaomba Watanzania, hususan waliopo jijini Nairobi nchini Kenya na maeneo ya jirani, kujitokeza kuwaunga mkono mabondia wetu wanapoiwakilisha nchi katika mashindano haya ya kimataifa.

Imetolewa na:

Makore Mashaga

Katibu Mkuu

Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT)

0/Post a Comment/Comments