Makamu wa Rais wa Tanzania Deogratius John Ndejembi amewasili Mkoani Arusha leo Jumatatu Oktoba 05, 2026 kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla pamoja na Viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi CCM na Serikali kwa ajili ya kufungua Mkutano wa 46 wa Chama cha Wasimamizi wa Kodi wa Jumuiya ya Madola (CATA).
Mkutano huo utafanyika Oktoba 06 mpaka 09 katika Ukumbi wa Gran Melia Jijini Arusha, ukiwakutanisha Viongozi na wataalam wa masuala ya kodi zaidi ya 400 kutoka Mataifa 48.



Post a Comment