POLISI DAR KUIMARISHA ULINZI MCHEZO WA SIMBA NA YANGA

..........

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam lipejipanga kuimarisha ulinzi na usalama katika mchezo wa soka wa ligi kuu Tanzania bara unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 10 Oktoba, 2026 kuanzia saa 1:00 usiku kwenye uwanja wa Uhuru Temeke Jijini Dar es salaam kati ya timu ya Simba na Yanga zote za Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa na Kaimu Kamanda wa Jeshi hilo Faustine Mafwele amesema Jeshi hilo linatambua kuwepo kwa mchezo huo, hivyo ulinzi umeimarishwa na utaendelea kuimarishwa kwa kushirikiana na wadau wote.

Amewasisitiza mashabiki, wapenzi na wadau wote wa soka kujiepusha na vitendo vyovyote vile vilivyo kinyume na sheria, kanuni na taratibu za mkusanyiko wa mchezo mkubwa kama huo.

0/Post a Comment/Comments