Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amezitaka taasisi za kidini kuendelea kuhamasisha amani, umoja na utulivu, akisisitiza kuwa ni misingi muhimu ya maendeleo na ustawi wa wananchi
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, Oktoba 21, 2026, alipokutana na Mhasham Baba Askofu Lameck Paul Ndomba, Askofu wa 11 wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar, Ikulu Zanzibar.
Amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali na taasisi za kidini katika kuimarisha upendo, mshikamano na kutekeleza shughuli za maendeleo kwa manufaa ya wananchi.
Kwa upande wake, Askofu Ndomba amesema yupo tayari kushirikiana na Serikali katika kuhamasisha amani, maelewano na maridhiano, akieleza kuwa jamii yenye amani na umoja ina mazingira bora ya kushiriki katika shughuli za maendeleo.









Post a Comment