RAIS DKT. MWINYI ATOA WITO WA KUIMARISHA UFADHILI WA UHIFADHI WA BIOANUAI

.......

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameshiriki majadiliano ya ngazi ya juu kuhusu ufadhili wa bioanuai na uwekezaji unaozingatia mazingira, pembezoni mwa Mkutano wa Viongozi kuhusu Bioanuai (COP17) mjini Yerevan, Armenia. Katika majadiliano hayo, ameeleza kuwa Tanzania inalenga kupata takriban dola za Marekani milioni 41 kupitia mifumo ya kimataifa ya ufadhili wa mazingira kwa ajili ya kutekeleza miradi ya uhifadhi na urejeshaji wa mifumo ya ikolojia.

Rais Dkt. Mwinyi amehitimisha ziara yake ya kikazi nchini Armenia leo, tarehe 16 Oktoba 2026, baada ya kushiriki mkutano huo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika ziara hiyo, ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. James Kinyasi Millya, Balozi wa Tanzania nchini Urusi anayewakilisha pia Armenia, Mhe. Fredrick Ibrahim Kibuta, pamoja na viongozi na maafisa mbalimbali wa Serikali.








 

0/Post a Comment/Comments