RAIS MPYA WA IPU AIPA TANO MALIASILI

..........

📌 Zaidi ya wageni 2,000 wa IPU watembelea vivutio vya utalii 

Na Sixmund Begashe, Arusha

RAIS mpya wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Australia Mhe. Milton Dick

ametembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii katika Mkutano wa 153 wa IPU na kupongeza kwa kazi nzuri za Uhifadhi na Utalii. 

Katika banda hilo Mhe. Dick alipokelewa na wataalam wa Wizara hiyo pamoja na wadau wa Utalii na kisha kupata picha ya pamoja. 

Akizungumzia ujuo wa ugeni huo mkubwa kwenye Banda la Maliasili na Utalii, Ofisa Utalii Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bi. Ester Solomon amesema ni heshma kubwa na kuwa ni hatua muhimu ya kujitangaza zaidi kimataifa. 

Bi. Solomon ameongeza kuwa mwitikio wa wageni wa Mkutano huo kutembelea banda hilo na kwenye vivutio vya utalii nchini ni mkubwa. 

"Wajumbe waliohudhuria mkutano huu ni zaidi ya 2,200 na walio tembelea vivutio vyetu ni takribani wote, maana wapo walio kwenda kwenye Hifadhi, Makumbusho za hapa Arusha pamoja na sehemu za Utamaduni," alisema Bi. Solomon.

Naye Mkwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Utalii Wazawa Tanzania Bw. Samuel Diah, amesema wamefanya kazi kubwa ya kuwasafirisha zaidi ya wageni 2,000 wa Mkutano huo sehemu mbalimbali za vivutio vya utalii. 

Bw. Diah ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuwajali wadau wa Utalii kwa kuwatengenezea fursa mbalimbali hususani ya kushiriki kwenye Mkutano huo.




 

0/Post a Comment/Comments