RC CHALAMILA "MAWASILIANO NI FURSA YA MAENDELEO



.....

-Azindua duka la kisasa Airtel makao makuu, amepongeza uwekezaji unaofanywa na Airtel.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Octoba 16, 2026 amezindua duka la kisasa la Airtel makao makuu Kinondoni Jijini Dar es Salaam ambapo amesema "Mawasiliano ni Fursa ya Maendeleo"

RC Chalamila amesema kwa kuwa Mkoa huo watu wanatafuta fursa mbalimbali za kibiashara, viwanda na teknolojia hivyo mtandao wa Airtel umewezesha upatikanaji wa fursa hizo ambazo zina mchango mkubwa katika makuzi ya uchumi wa Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Aidha Mkuu wa Mkoa amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi shupavu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan imedhamiria kujenga uchumi wa kidigitali kuelekea Dira ya Taifa 2050. Serikali imedhaidhinisha malipo mengi kufanyika mtandaoni na Airtel ni kinara katika huduma hizo. "Napongeza Airtel kwa maboresho ya huduma mmeleta 4G na 5G hongereni sana"

Vilevile Mhe Chalamila amepongeza Aitel kwa kutoa gawio la Tsh Bilioni 65.48 kwa Mhe Rais mwaka huu na kufikisha zaidi ya bilioni 350 tangu mwaka 2019.

Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa Airtel Tanzania Bw Charles Kamoto amesema Airtel inashirikiana na Serikali kwa kiasi kikubwa kupitia "Public Private Pertineship" ambapo Serikali ina hisa 49% hivyo ametoa rai kwa wananchi kutumia fursa za kidigitali kufanya biashara, kujifunza na kuongeza kipato.





 

0/Post a Comment/Comments