SHAHIDI WA MAJI YATOA TATHMINI YA MATOKEO YA MRADI WA UWAJIBIKAJI WA MAJI

Mratibu wa  mradi wa Uwajibikaji wa Maji Tanzania kutoka Shahidi wa Maji Mwajuma Basho, akizungumza  kwenye warsha maalum ya kujadili tathmini ya matokeo ya Programu ya uwajibikaji wa maji ambayo imewakutanisha wanajamii,pamoja na viongozi ambayo imefanyika tar Oktoba 17,2026 jijini Dar es salaam
Meneja wa Program kutoka Shahidi wa Maji Pendo Yera  akizungumza  kwenye warsha maalum ya kujadili tathmini ya matokeo ya Programu ya uwajibikaji wa maji ambayo imewakutanisha wanajamii,pamoja na viongozi ambayo imefanyika tar Oktoba 17,2026 jijini Dar es salaam 
Mhandisi wa Usambazaji na Matengenezo ya maji DAWASA Mkoa wa Tabata Mhandisi Daniel Sabuni akizungumza  kwenye warsha maalum ya kujadili tathmini ya matokeo ya Programu ya uwajibikaji wa maji ambayo imewakutanisha wanajamii,pamoja na viongozi ambayo imefanyika tar Oktoba 17,2026 jijini Dar es salaam. 
Diwani wa Kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto akizungumza  kwenye warsha maalum ya kujadili tathmini ya matokeo ya Programu ya uwajibikaji wa maji ambayo imewakutanisha wanajamii,pamoja na viongozi ambayo imefanyika tar Oktoba 17,2026 jijini Dar es salaam. 
Nantaika Maufi ambaye ni mdau wa harakati za maji mkoa wa Dar es salaam akichangia jambo kwenye warsha maalum ya kujadili tathmini ya matokeo ya Programu ya uwajibikaji wa maji ambayo imewakutanisha wanajamii,pamoja na viongozi ambayo imefanyika tar Oktoba 17,2026 jijini Dar es salaam. 
 Baadhi ya wadau wa maji walioshiriki wenye warsha maalum ya kujadili tathmini ya matokeo ya Programu ya uwajibikaji wa maji ambayo imewakutanisha wanajamii,pamoja na viongozi ambayo imefanyika tar Oktoba 17,2026 jijini Dar es salaam (Picha na Mussa Khalid)

.......................

NA MUSSA KHALID

Shirika lisilo la kiserikali la Shahidi wa Maji limesema mradi wa uwajibikaji uliokuwa ukitekelezwa katika Kata ya Vingunguti, jijini Dar es Salaam, umefanikiwa kwa kiwango kikubwa kwa kufikia asilimia 70 ya matokeo yaliyokusudiwa. 

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Mratibu wa  mradi wa Uwajibikaji wa Maji Tanzania kutoka Shahidi wa Maji Mwajuma Basho, wakati akizungumza  kwenye warsha maalum ya kujadili tathmini ya matokeo ya Programu ya uwajibikaji wa maji. 

Mwajuma amesema kuwa kupitia mradi huo ambao umeanza 2023 na kumalizika mwaka huu wamejikita katika kuhakikisha tafiti ambazo wamezifanya awali zinaleta tija kulingana na malengo waliyojiwekea.

Amesema kuwa mradi huo umekuwa na malengo mbalimbali ikiwemo ya kufikisha elimu kuhusiana na uwajibikaji wa maji kwa kutoa taarifa haki na majukumu ya wananchi na Mamlaka,lakini pia kuhakikisha jamii wanazofanya nazo kazi zinapata uhakika wa maji. 

Lengo lingine amelitaja kuwa lilikuwa ni kuhakikisha matokeo ya uwajibikaji wa maji yanatumika na Mamlaka kwa ajili ya kuleta mabadiliko ambayo wamekuwa wakiyatarajia.

Kuhusu Tathmini amesema imekuwa na matokeo chanya kwa kutokana na ushirikiano wanaoupata kutoka kwa mamlaka DAWASA na hata MORUWASA kuhakikisha wanajibia changamoto za upatikanaji wa maji zinazowakumba wananchi katika maeneo yao.

"Tunazisisitiza Mamlaka ziendelee kushirikiana na wanajamii katika kupata suluhisho za changamoto zinazoweza kutatulika haraka na za muda mrefu ni vizuri zikatoa taarifa endapo utachukua muda mrefu.

Awali Meneja wa Program kutoka Shahidi wa Maji Pendo Yera amesema warsha hiyo imetoka na maazimio ambayo yatachukuliwa na kufanyiwa kazi na Mamlaka husika ili changamoto zote zinazoikabili jamii hususani za maji ziweze kupatiwa ufumbuzi. 

Pia ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa jamii kuendelea kushiriki katika matukio mbalimbali yanaratibiwa na Shahidi wa Maji ikiwemo.kutoa taarifa zitakazowezesha kupata majibu ya changamoto zinazotokea katika maeneo ya. 

Akizungumzia jitihada za kutatua changamoto za huduma za maji Vingunguzi ambazo zimeibuliwa na wanajamii katika warsha hiyo Mhandisi wa Usambazaji na Matengenezo ya maji DAWASA Mkoa wa Tabata Mhandisi Daniel Sabuni amewapongeza Shahidi wa Maji kwa kuingia mtaani na kufanya tafiti ya kuibua changamoto zinazowakumba jamii na kutafuta suluhisho katiia uwajibikaji.

Pia amewasisitiza wananchi kuwa watulivu kwani wananchi watafikishiwa huduma za maji na wenye changamoto zitafanyiwa kazi ili waweze kupata huduma za maji kwa wakati.

Naye Diwani wa Kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto amesema utafiti walioufanya Shahidi wa Maji Vingunguti ni wakweli kwani umeibua changamoto zinazowakumba wakazi wa vingunguti huku Nantaika Maufi ambaye ni mdau wa harakati za maji mkoa wa Dar es salaam ameeleza kuwa ili kukabiliana na changamoto ya maji waliungana wanawake mkoa wa Dar es salaam na kuzindua kisima cha maji kwa lengo la kuwasaidia wananchi.


0/Post a Comment/Comments